WAZIRI wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba ametoa mapendekezo ya kufanya marekebisho kwenye sheria ya ongezeko la thamani kwa kusamehe kodi kwenye mafuta ya kura yanayozalishwa nchini kwa kutumia mbegu zinazo zalishwa nchini ili kuweka unafuu wa bei ya bidhaa hiyo.
–
“Sambamba na kusamehe kodi hiyo kwenye malighafi na vifungashio vinavyotumika kwenye uzalishaji, lengo la msamaha huu ni kuleta unafuu wa bei ya mafuta ya kula iliyopanda kutokana na mdororo wa uchumi,” amesema Waziri Nchemba.
Pia Waziri amependekeza Bungeni kupunguza kiwango cha kodi ya zawadi kwa mshindi (Incoming Tax on Winning) kutoka asilimia 15 hadi 10 kwenye michezo ya kubahatisha ya ubashiri wa michezo (Sports Betting) ili kuongeza mapato ya serikali.
–
“Uchambuzi umebainisha kwamba endapo serikali itapunguza kiwango cha kodi hadi asilimia 10, mapato ya serikali yatoongezeka kutoka Sh bilioni 4 hadi Sh bilioni 5.2 kutokana na kiwango cha watu wengi zaidi kushiriki katika michezo hiyo,” Waziri Nchemba.