Mali za Wakili Median Mwale aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi zimetaifishwa na Serikali na kukabidhiwa kwa Ofisi ya Hazina.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga, aliyeongozana na baadhi ya maofisa wa Hazina akiwamo Benezeth Ruta ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, walizikagua mali hizo yakiwamo magari sita ya kifahari nyumba mbili na shamba vyote vyenye thamani zaidi ya Sh bilioni 1.197 na zitapangiwa matumizi baadaye.
DPP alisema katika kesi ya maombi ya jinai namba 100 ya mwaka jana iliyokuwa kati ya DPP dhidi ya Mwale, Aprili 14, mwaka huu Mahakama Kuu ilitoa amri ya kutaifishwa kwa mali hizo.
Mwale ambaye ni wakili maarufu jijini Arusha, alitiwa hatiani baada ya kukiri makosa 30 yakiwamo ya kutakatisha fedha haramu na kughushi.
GOOD NEWS YA DREAMLINER KUTOKA TANZANIA MPAKA CHINA