Kamati ya Kudumu ya Bunge, hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imetoa muda wa miezi 3 kwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenda kufanya ukaguzi Maalumu katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita baada Ya Kubainika ubadhilifu wa zaidi ya Tsh.Bilioni 3.
Akizungumza mbele ya kamati hiyo Bungeni Dodoma iliyokutanisha watumishi wa Halmshauri ya Nyang’hwale na wa CAG, Makamu Mwenyekiti wa LAAC , Abdallah Chikota amesema ofisi ya CAG imetoa hati mbaya kwa Halmashauri hiyo baada ya kutoridhishwa na matumizi ya fedha za Serikali.