Wafanyabiashara wanne na madereva wa madini ya dhahahu wamehukukiwa kifungo cha miaka 20 jela ama kulipa faini ya Milioni 341 baada ya kukiri makosa ya kusafirisha madini yenye thamani ya Bilioni 2.9.
Katika mgawanyo wa Milioni 341, kiasi cha Milioni 125 ni faini na Milioni 216.5 ni fidia wanayotakiwa kulipa kutokana na kuisababishia Serikali hasara.
Washitakiwa hao ni Faisal Ally (31) ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Kariakoo, Isack Shija (28) Dereva na mkazi wa Kiluvya na Abdulkarimu Doshi (25) Msimamizi wa Kampuni ya FAA Truck Ltd na Mkazi wa Gachuriro Rwanda.
Wengine ni Abas Said (23) dereva na mkazi wa Mtongani, Nassoro Sleyyum (23)dereva na mkazi wa Tandika na Ahmed Abubakari (32) mfanyabiashara na mkazi wa Upanga.