Kampuni ya The Network inayoendesha mchezo wa bahati na nasibu wa Tatu Mzuka leo October 18 2018 imetoa milioni 20 kusaidia ujenzi wa wodi za watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Katika tukio la makabidhiano lililofanyika katika hospitali ya moyo ya Jakaya Kikwete, Mhimbili, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof Mohamed Janabi aliishukuru The Network kwa mchango wao na kusisitiza zaidi umuhimu wa watoto kuwa na wodi yao ambapo kwa sasa wanatumia wodi moja na watu wazima. Aliongeza pia kwamba itakuwa wodi ya kwanza nchini inayotoa huduma kwa watoto peke yao kwa sababu takribani asilimia 70% ya upasuaji unaofanyika hospitalini hapo ni wa watoto.
Professor Janabi alielezea pia kwamba tangu mwaka 2015 taasisi hiyo ilipoanzishwa wamewahudumia wagonjwa takribani 8000 ambapo kati ya hao 519 wamefanyiwa upasuaji wa moyo (open-heart surgery) huku 370 wakifanyiwa upasuaji mdogo jambo ambalo linaonyesha umuhimu mkubwa wa kujenga majengo zaidi kusaidia wagonjwa wanaohitaji huduma ya kulazwa.
Tatu Mzuka imekuwa mstari wa mbele kubadili maisha ya watanzania sio tu kwa kutoa zawadi kubwa kwa washindi wa jackpot lakini pia katika ushiriki wake katika shughuli mbalimbali za kusaidia jamii.
“Tangu tulipoanza mwaka 2017, tumesaidia shughuli za kijamii katika sekta mbalimbali kama vile afya, mazingira na elimu. Kupitia ujenzi huu, tunaamini kwamba maisha ya baadaye ya watoto wetu yatakuwa katika mikono salama. Katika kipindi cha ugonjwa inabidi tuwatengenezee mazingira mazuri ya kupona. Kwa niaba ya The Network tunawapongeza kwa kufanya kazi hii kwa ufanisi na mafanikio makubwa kila siku” alihitimisha Mkurugenzi wa Mawasiliano wa The Network Bwana Sebastian Maganga
Idadi ya watoto wenye matatizo ya Moyo waliotibiwa tangu JKCI ianzishwe, Bonyeza Bonyeza play hapa chini kutazama