Rais wa Brazil Jair Bolsonaro ameambukizwa virusi vya corona kwa mujibu wa vipimo vya Madaktari, Rais huyo amesema licha ya kwamba ana dalili za homa na joto kali lakini yupo imara na anaamini virusi hivyo havitomfanya awe hoi na kulazwa Hospitali na kwamba atapona hivi karibuni.
Rais huyo aliwahi kunukuliwa akipuuza miongozo ya kujikinga na virusi vya corona ikiwemo kugoma kabisa kuvaa barakoa huku akitoa kauli za kuudharau ugonjwa huo kwa kuuita ‘Mafua ya Kawaida’.