Msanii wa Bongofleva Gigy Money ameomba kufunguliwa adhabu yake ya miezi 6 baada ya Rais Samia Suluhu kusema Vyombo vya Habari vilivyofungwa vifunguliwe ila wafuate sheria na miongozo ya Serikali.
“Wizara ya Habari, nasikia kuna Vyombo vya Habari mmevifungia, sijui viji- TV vya mikononi vile ‘online’, vifungulieni lakini wafuate sheria na miongozo ya Serikali, tusiwape mdomo wa kusema tunabinya Uhuru wa Vyombo vya Habari, tusifungie tu kibabe” Rais Samia Suluhu Hassan
Baada ya Samia Suluhu Hassan kusema hivyo msanii Gigy Money amecomment’ kwenye post iliyopost kwenye Millard Ayo “Na mimi nifunguliwe jamani, kazi inaendelea mama“.