Huenda utofauti wa tamaduni na mazoea ya watu inafanya baadhi ya vitu pia kutofautiana.. zipo story za watu kula mbwa na wanyama wengine, huku kwetu sio kawaida.
Kumbe China kuna soko la nyama ya punda? Kuna maeneo ukienda utakuta punda wanatumiwa kubebea mizigo basi, lakini kwa China punda ni nyama yenye soko kubwa tu.
Eneo la Maraigishu mji wa Naivasha, Kenya kuna story ya ujenzi wa eneo la kiwanda cha machinjio ya punda kuelekea kukamilika, ambapo tayari nyama hiyo ina soko la uhakika ndani ya China.
Msimazi wa ujenzi huo Stephen Kairuki amesema ujenzi huo umekamilika kwa 80%, eneo hilo litakuwa na Ofisi za kiwanda hicho pamoja na maabara maalum ya kupima nyama kabla ya kupakiwa, pia kutakuwa na mashine maalum ya kuchinjia punda na kuwachuna ngozi.
Fundi huyo amepata nafasi ya kufanya mahojiano na ripota wa millardayo.com ambapo amesema wanakijiji wa eneo hilo watapewa punda wawili wa kufuga; “sio kila mtu bali wakulima wa eneo hili watapewa punda wa kike na wakiume, wakulima wanatarajiwa kuwafuga na kuwauzia kiwanda hicho kila wanapokomaa“
Kutokana na mahitaji ya soko la nyama hiyo China, kwa siku watatakiwa kuchinjwa punda 70, mbali na uhitaji wa nyama pia kuna wafanyabiashara waliotoka Marekani ili kuingia makubaliano ya kununua ngozi ya mnyama huyo kwa ajili ya kutengenezea dawa ya vipodozi vya wanawake.
Kingine kitakachowanufaisha wanakijiji kutoka kwenye kiwanda hicho ni huduma ambazo watasogezewa kutokana na mradi huo kuwa kwenye kijiji hicho ikiwemo huduma ya maji, hospitali na ajira kwa zaidi ya vijana 100.
Ufunguzi wa mradi huo utafunguliwa ndani ya kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa.
Hizi ni baadhi ya picha kutoka Kenya kwenye mradi huo.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook