Ikiwa leo Mei 1 2020 ni siku ya kuzaliwa kwa mpendwa wetu Ruge Mutahaba, sasa Hapa Mbunge Nape Nnauye amefunguka kupitia Clouds360 ya Clouds TV kazungumza machache anayokumbuka kutoka kwa Ruge
Alikuwa Rafiki yangu mshikaji wangu, ni mshikaji ambae alikuwa ni zaidi ya ndugu yangu na niliwahi kufundishwa kwamba Ndugu sio mpaka uzaliwe nae tumbo mmoja
‘Alikuwa amenizidi kwa miaka 5 kwahiyo alikuwa akiniita Mdogo wangu nilikuwa sishangai akiwa na January Makamba, kwakweli Ruge alikuwa hapendi kufanya shughuli za siku ya kuzaliwa mara nyingi alikuwa anapenda kufanya zaidi kazi’
Ruge alikuwa mchapakazi sana sana, nakumbuka kuna siku tuliwahi kumuita Dodoma nikiwa na January Makamba tulimsema pale anapokosea na alikuwa anatusikiliza ndio kitu pekee ambacho najivunia Ruge kwani alikuwa ni mtu wa kusikiliza mawazo mbalimbali’- Nape
‘Ruge alikuwa anaamini akikutana mtu hata kwa dakika mmoja anataka asababishe mabadiliko na kama kuna sehemu nakosea basi ananikosea sana’- Nape
‘Ruge alikuwa aamini sana kwenye solution kupitia siasa mimi alikuwa ananiambia Nape nyie Wanasiasa mmetuharibu sana yeye alikuwa anasema hatuwezi kutafuta solution nje ya Siasa na nadhani ndio maana akaanzisha Fursa kwamba tuwafanye watu wasidhani kwamba shida zao zote zitamalizwa na Bunge, zitamalizwa na Serikali’- Nape
‘Ruge alikuwa ni mtu wa kutafuta Majibu na kama kuna jambo amemos basi lazima akuambie hakuna jambo linalokwama kwa Ruge lazima jambo alibebe liwe lake hakikisha kila kitu kinaenda sawa’- Nape