Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewaachia huru madiwani 29 na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uharibifu wa mali baada ya upande wa mashtaka kuondoa shauri hilo mahakamani.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Desidery Kamugisha ameamua kufuta shauri hilo chini ya kifungu cha 91 baada ya upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na wakili wa Serikali Blandina Msawa kuielezea mahakama kuwa haina haja yakuendelea na shauri hilo.
ULIKOSA JOSHUA NASSARI KUKATAA KUJADILI WANAFUNZI KUFUKUZWA UDOM? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI