Jeshi la polisi kwa kushirikiana na mamlaka yakupamabana na kudhibiti dawa za kulevya nchini wamekamata nakuteketeza kwa moto madawa yakulevya aina ya bangi magunia 160 ambayo ni zaidi ya tani mbili walizozikamata zikiwa zimehiadhiwa nyumbani kwa watuhumiwa wawili katika kijiji cha Engalauni wilayani Arumeru mkoani
Kaimu kamishna jenerali wa mamlaka yakupamabana na dawa za kulevya nchini James Kaji amesema katika operesheni hiyo waliyoifanya wamefanikiwa kuwakamatwa watu wawili na taratibu za kisheria zitakapokamilika watapelekwa mahakamani