Wakati moto ukiendelea katika mlima Kilimanjaro, Serikali kupitia katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utakii Prof Eliamani Sedoyeka imeliomba Jeshi la Wananchi(JWTZ)kuongeza nguvu ili kuweza kuudhibiti moto huo ambao unaendelea kusambaa kwa kasi kutokana na upepo mkali.
Ndege ya Shirika la hifadhi za Taifa (Tanapa) iliyokuwa imebeba kamati ya usalama ya Mkoa wa Kilimanjaro kuelekea eneo la Karanga-Baranko eneo ambalo moto unawaka, imeshindwa kufika eneo la tukio kutokana na hali ya hewa na Moshi mkali unaotokana na moto huo.