September 14 na kusogezea karibu yako na moja kati ya stori nzuri za ukuwaji wa kiteknolojia. Hii ni stori kutoka mymodernmet.com licha ya kuwa ni stori ya muda ila inawezekana ilikupita mtu wangu, haya ni maendeleo mengine ya kiteknolojia.
Licha ya kuwa haikuwahi kushinda tuzo ya gari yenye mvuto Terrafugia ilitajwa kuwa ni moja kati ya gari zitakazotumika miaka ya baadae. Terrafugia kwa mara ya kwanza ilipaa March 5 2009 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Plattsburgh New York.
Mtengenezaji wa Terrafugia gari inayopaa Carl Dietrich alinukuliwa akisema mabadiliko ya gari hiyo yalianza kufanyiwa uchunguzi toka 1918, licha ya kuwa yapo yaliyowahi kutengenezwa na kufanyiwa majaribio kabla ya hili lakini hii imekuwa ya kwanza kuthibitika na kukubalika.
Ina uwezo wa kubeba watu wawili, ina uwezo wa kupaa maili 450 lakini inatajwa kuwa na uwezo wa kubadilika kutoka ndege kuwa gari ndani ya sekunde 30 tu. Bei yake ilikuwa inatajwa kuwa dola 194000 ambayo ni zaidi ya milioni 420 za kitanzania kwa thamani ya dola kwa sasa.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos