HABARILEO
Kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa unaofanyika leo zilimalizika jana kwa mbunge wa Arusha Godbless Lema wa CHADEMA na Mbunge wa Kwela Ignas Malocha kulazimika kutumia silaha za moto kujihami baada ya kukumbana na magenge ya vijana wa mitaani kuwafanyia fujo wakitokea katika kampeni za uchaguzi.
Kutokana na mtafaruku huo,Lema alilamizika kufyatua risasi mbili hewani baada ya kukutana na genge hilo wengi wao wakiwa watoto wa mitaani ambao walikua wakifanya vurugu kwa kurusha mawe na kupiga watu kwa mapanga na bisibisi maeneo ya karibu na Hotel ya New Arusha.
Lema alisema amenusurika kifo kwani vijana hao walikua wakipiga watu waliokua wanakutana nao barabarani na yeye alikua akitokea kwenye kampeni nyakati za jioni.
Alisema alilazimika kufyatua risasi mbili hewani ambazo hata hivyo vijana hao hawakuogopa na kulizunguka gari lake ambapo yeye alilazimika kushuka na kukimbia kujificha ndipo vijana hao wakavunja kioo cha gari cha pembeni.
Kwa upande wa mbunge wa Sumbawanga Ignas Mlocha alinusurika kujeruhiwa baada ya gari lake kupondwa mawe na vijana wanaodaiwa ni wafuasi wa vyama vya upinzani na alilazikika kufyatua risasi ili kujiwinda.
HABARILEO
Wakati shinikizo lakumtaka Rais Jakaya Kikwete awawajibishe viongozi wanaotuhumiwa katika sakata la akaunti ya Escrow,imeelezwa kuwa wengi wao wanaishi kwa hofu kwani hawajui hatima yao hadi sasa.
Hofu hiyo imetawala zaidi baada ya Marekani kushinikiza Serikali ya Kikwete ifanye uamuzi wa suala hilo kama alivyoahidi Desemba 9 mw aka huu wakati wa maadhimisho ya sikukuu za Uhuru vinginevyo watasitisha misaada yao.
Msaada ambao Marekani umetishia kuzuia ni trilioni 1.1 sawa na dola za Marekani milioni 700 unaohusu mradi wa pili wa mfuko wa changamoto za Milenia MCC ambapo unahusu masuala ya maji,umeme nk.
Shinizo la nchi hiyo la kutaka rais achukue hatua za haraka katika nchi suala hilo linatokana na kushamiri kwa vitendo vya rushwa kwa muda wa miaka saba mfululizo.
Kwa mujibu wa kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali PAC ni kwamba viongozi wanaotuhumiwa katika sakata hilo ni Mwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema.
MWANANCHI
Mganga wa tiba za asili Omar Kikukwa mwenye miaka32 Wilayani Kilindi anashikiliwa na polisi kwa kuwachoma moto wateja wake na kusababisha mmoja wao kufariki dunia.
Aziza Hassan mmoja wa wnaafamilia walionusurika katika mkasa huo alisema mama yake pamoja na watoto wake wawili walipelekwa kwa mganga wa kienyeji na baba yao wa kufikia kwa ajili ya kufanyiwa tambiko.
Alisema kuwa walipofika kwa mganga huyo na kuanza kufanyiwa dawa ambapo ilifanyika ndani ya shimo ambalo liliezekwa kwa nyasi juu yake na kuachwa nafasi ndogo kwa ajili ya kuingilia ndani ya shimo waliloambiwa ndipo dawa inatakiwa kufanyika huku baba yao akibaki nje na mganga.
Alisema baada ya muda walidhani mganga ameshamaliza na aliwajibu dawa bado inaendelea na gafla mganga huyo aliwasha moto mkubwa na kuanza kuwaka ndipo akawaamrisha watoke shimoni huku moto ukiendelea kuwaka hadi mlangoni.
Alisema baada ya moto kupungua walitoka huku wenzake wakiwa hawajiwezi kabisaambapo baba yakena mganga waliwakataza kwenda hospitali na kuwaambia kuna daktari wao anakwenda kuwatibu katika kijiji cha jirani na hapo huku mwenzao mmoja akipoteza maisha.
Kwa sasa mganga huyo anashikiliwa na polisi kwa kosa lakusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine watatu kwa moto.
MTANZANIA
Aliyekua mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa kijiji cha kwa sadala Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro kwa tiketi ya Chamacha Mpinduzi CCM Ernest Munisi mwenye miaka 60 amefariki dunia gafla hivyo uchaguzi kwenye kijiji hicho kuahirishwa.
Kwa mujibu wa barua toka kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo Alex Kombe alisema uchaguzi huo utaahirishwa kwa siku zisizopungua kumi ili kutoa nafasi kwa CCM kumteua mgombea atakayechukua nafasi hiyo.
“Kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi wa Serikali za mitaa kifungu cha nne kianeleza kuwa endapo mgombea atafariki,uchaguzi hautafanyika na utaahirishwa ili kutoa nafasi kwa chama husika kumtafuta mgombea mwingine ndani ya siku kumi,”alisema.
Munisi alikua mwenyekiti wa kijiji cha kwa sadala kwa vipindi viwili ambapo ameacha mke na watoto watano.
MTANZANIA
Mwanamke asiyejulikana anayetumia jina la mwigizaji maarufu wa Bongo Movie Jackline Wolper sasa amebadili mbinu na kuanza kulenga kuwatapeli wanasiasa maarufu.
Miongoni mwa wanasiasa wanaonekana kulengwa na mwanamke huyo tapeli ni wale kutoka Chama cha demokrasia CHADEMA na juzi alimpigia muhariri mkuu wa Kampuni ya New habari Absoloam Kibanda na kumwomba namba za wanasiasa watatu wa Chadema.
Mwanamke huyo ambaye namba yake ya simu imesajiliwa kwa jina la Jackline Masawe ambalo ni jina sahihi la mwigizaji huyo alianza kwa kumtumia Kibanda ujumbe mfupi kupitia mtandao wa facebook akiomba kupatiwa namba za wanasiasa hao.
Kibanda alipomdadisi sababu za kumtafuta alisema alikua na jambo alifikiria lingeweza kumsaidia katika shughuli zake na aliomba apewe namba za John Mnyika,Godbles Lema pamoja na Joseph Mbilinyi.
Kwa mujibu wa Lema alianza kupatwa na wasiwasi kuhusu uhaliasia wa tapeli huyo baada ya kupokea ujumbe wa maandishi ukiombwa kusaidiwa kiasi cha 250,000 ili aweze kukabiliana na matatizo yanayomkabili.
NIPASHE
Askari Mkoani Kilimanjaro imewatia mbaroni askari polisi sita wa kituo cha Polisi Himo kwa tuhuma za kuwasindikiza wahalifu kutoka nchini Kenya na kuingia Tanzania kinyume na sheria.
Imeelezwa kuwa wahalifu hao ni wezi wa magari walioingia nchini na kukamatwanabaadaye kuwahonga askari na kuachiwa kabla ya kukamatwa tena mjini Moshi.
Wahalifu hao inadaiwa walikua na magari mapya mawili kutoka nchini Kenya yaliyokua hayana kibali cha TRA,Bima wala vibali vya kuingia nchini.
Kamanda wa Polisi Mkoani humo Godfrey Kamwela amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema hawezi kuwataja majina kwa sasa wakati upelelezi unaendelea.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook