Michezo

Fedha walizotumia Barcelona kuwaleta marafiki Neymar kwenye utambulisho wake

on

Screen Shot 2014-10-10 at 9.16.37 AMUsajili wa kumleta Neymar Dos Santos katika klabu ya FC Barcelona uligubikwa na utata mkubwa na hatimaye ulimgharimu Sandro Rosel kazi yake ya urais katika klabu hiyo ya Catalunya.

Mwanzoni ilitangazwa kwamba ada ya €57m ililipwa kwa usajili wa Neymar, lakini katika matukio ya hivi karibuni yanaonyesha dili hilo la uhamisho limeiigharimu klabu zaidi ya €100k, Rosell bado chini ya uchunguzi kutokana na tuhuma hizi.

Gazeti la Cadenas Ser  limetoa taarifa kwamba Rosell amemwambia Jaji wa kesi yake wiki hii kwamba klabu yake ililipa kiasi cha €300,000 kuwasafirisha marafiki wa Neymar kutoka Brazil mpaka Barcelona kwa kutumia ndege binafsi katika utambulisho wa Neymar.

Kundi la marafiki wa Neymar maarufu kama ‘The ‘Toiss’ wamekuwa na Neymar tangu utotoni katika mitaa ya jiji la Sao Paulo, na wamekuwa wakimtembelea Neymar jijini Barcelona, lakini sasa ni mchezaji mwenyewe anayewalipia washkaji zake.

 

Tupia Comments