Mwanamuziki mkongwe Koffi Olomidé amepatikana na hatia katika kesi ubakaji wa mmoja wa wanengeuaji wake alipokuwa na miaka 15. Koffi amehukumiwa miaka miwili gerezani na mahakama ya Ufaransa akiwa hayupo, baada ya kukosa kufika mahakamani.
Inaripotiwa kuwa uamuzi huo uliofanywa na Mahakama unaeleza kuwa nyota huyo wa Congo atakamatwa endapo atafanya uhalifu mwingine, Koffi Olomidé mwenye umri wa miaka 62, aliagizwa alipe Euro 5,000 sawa na zaidi ya shilingi Milioni 13 za Kitanzania kwa madhara aliyomsababishia mnenguaje wake huyo wa zamani.
Inaelezwa kuwa wanenguaji wanne waliokuwa wakimfanyia kazi Koffi wameiambia Mahakama kwamba aliwanyanyasa kingono mara kadhaa kati ya mwaka 2002 na mwaka 2006 wameeleza kuwa unyanyasaji huo ulifanyika katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Ufaransa.
VIDEO: PASCAL WA BSS AANZA SAFARI YAKE, RC MAKONDA AMKABIDHI HATI ZA KUSAFIRIA