Michezo

Yanga ndiyo mabingwa TZ Bara.. leo ni headlines za mchezaji wao, Mrisho Ngassa

on

yanga-standd

Jopo maalum la makocha ambao huchagua wachezaji bora kwa kila mchezo kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara wametoa matokeo ya wachezaji waliochaguliwa kuwa bora kwenye ligi hiyo kwa mwezi April.

Mshambuliaji wa Yanga na timu ya Taifa, Mrisho Ngassa amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom ya mwezi April.

Ngassa ametajwa kuwa mshindi katika nafasi hiyo, wenzake ambao walikuwa wakishiriki ni pamoja na mchezaji Amos EdwardFrank Domayo na Emmanuel Okwi baada ya kupata alama nyingi za mchezaji bora kwa kila mchezo.

Mbali na Ngassa pia James Ambrose ametajwa kuwa mchezaji bora wa Ligi hiyo kwa mwezi March 2015.

Zawadi ambayo watapatiwa mastaa hao kila mmoja ni pesa kiasi cha Tshs. Mil. 1 kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments