Leo May 31, 2018 Mahakama imezuia matumizi ya vifungu kadhaa vya Sheria ya Mitandao iliyopitishwa na kusainiwa na Rais Kenyatta wiki mbili zilizopita.
Mahakama imevizuia vifungu 26 vya Sheria hiyo mpaka hapo shauri litakaposikilizwa, hatua hii inafikiwa baada vya chama cha Wanahabari na waendeshaji wa Blogu kufungua pingamizi.
Akitoa uamuzi huo Jaji wa Mahakama Kuu, Chacha Mwita amesema kuwa sheria hiyo ni kandamizi kwa haki za binadamu ikiwemo uhuru wa kujieleza.
Kesi hii imeahirishwa hadi Julai 18 mwaka huu.
MZEE WA UPAKO: ‘Yanga kapigwa Tatu, yani mwaka huu nina raha sana’