Leo June 20, 2019 Ni siku ya wakimbizi Duniani ni siku ya kutambua utu kwa vitendo na pia kushikamana na wakimbizi na jamii zinazowahifadhi ambapo Tanzania Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola ameongoza maadhimisho hayo Jijini DSM.
Na unukuu ujumbe wa Shirika la UNHCR “Tunapoadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa ya Wakimbizi Duniani, tunaheshimu ujasiri, ustahimilivu na uvumilivu wa wakimbizi zaidi ya Milioni 25 duniani kote ambao wamelazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na ukosefu wa amani, migogoro ya vita na jamii zinazoonyesha utayari wa kuwafungulia milango na kuwapokea”
Idadi ya watu waliolazimika kuyakimbia makazi yao hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2018 ni Milioni 70 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.
Tanzania inahifadhi Wakimbizi 312,152 kutoka nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tunawaalika wote kupiga hatua na wakimbizi yaani #StepWithRefugees kuelekea suluhisho la kudumu kwa tatizo la wakimbizi barani Afrika.