NI Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ambae leo Septemba 4, 2021 amekutana na Waandishi wa Habari kuzungumza mambo mbalimbali yakiwemo vitambulisho vya taifa “NIDA”.
“Watanzania wengi wanalalamika vitambulisho hatujapata tumeandikishwa, nitoe taarifa kwamba Serikali kupitia NIDA inaendelea vizuri na mchakato wa kutoa vitambulisho vya Taifa, mpaka sasa NIDA wameshatoa vitambulisho Milioni 9.4 na kati ya hivi Milioni 8.5 vimeshahakikiwa na vimepelekwa kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya kupewa Wahusika na kati ya vitambulisho milioni 8.5 Watanzania ambao wameshachukua vitambulisho vyao ni Milioni 7.2”
“Kuna vitambulisho Milioni 1.3 bado vipo kwenye Ofisi za Wasajili, sasa baadhi ya Watanzania ambao wanalalamika hawajapata vitambulisho vyao ni hawa ambao hawajaenda kuvichukua, Serikali inatoa wito kwa Watanzania wote ambao mlijisajili muende mkafuate vitambulisho vyao wavitumie” —asema Msemaji Mkuu wa Serikali