Duniani

Mnigeria huyu alikataa ofa ya kufanya kazi na bilionea Bill Gates, Sababu…

on

Katika stori zilizotrend kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na hii ya  kijana kutoka Nigeria, Chris Kwekowe ambaye ameripotiwa kuitolea nje ofa ya kufanya kazi kwenye kampuni ya Microsoft ya bilionea  Bill Gates na kusema kwamba watu wengi nchini kwake (Nigeria) hawana ajira hivyo hatoweza kukubali kufanya kazi hiyo badala yake ataendeleza biashara ya tovuti yake ya Slatecube ambayo aliianzisha kwa lengo la kuwasaidia  vijana kutafuta ajira kupitia mitandao.

Chris Kwekowe (23) amehitimu masomo ya Computer Science katika chuo kikuu cha Lagos State na alipata nafasi ya kukutana na Bill Gates baada ya kushinda tuzo ya mjasiriamali bora ya “Anzisha” na kupata zawadi ya Dola elfu 25,000 za Marekani.

Video: Dakika 30 za Mtanzania Hallen aliyetajwa FORBES kuwa Bilionea ajae>>>

Video: Changamoto anazokutana nazo Diana kwenye kambi ya Miss World Marekani>>>

Soma na hizi

Tupia Comments