Mshambuliaji wa Nigeria Emmanuel Emenike hivi karibuni aliifungia klabu yake bao lake la kwanza ikiwa imepita miezi mitatu alipofunga mara ya mwisho katika ligi ya Uturuki ambako anachezea klabu ya Fenerbace.
Emenike alifunga moja kati ya mabao mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya timu ya Karabuscorp na lilikuwa ni bao muhimu kwake kwani alikuwa hajafunga bao lolote kwa muda wa miezi mitatu.
Cha kufurahisha ni kwamba mshambuliaji huyu alifikia hatua ya kuamini kuwa hafungi kwa sababu amerogwa hali ambayo ilimfanya atafute msaada wa kiimani ambao aliupata hivi karibuni.
Emenike alikwenda kwa matabibu wa kitamaduni huko Uturuki ambao walimfanyia tambiko maalum la kumuondolea mkosi na siku chache baada ya tambiko hilo jamaa alifunga bao la kwanza baada ya kupita miezi mitatu bila kufunga goli lolote.
Nyota huyu hata hivyo amekanusha taarifa hizi japo zimesambaa nchini Uturuki ambako kila mtu anafahamu kuwa alilazimika kwenda kusaka msaada wa waganga ili avunje ukame wa mabao.
Emenike anaingizwa kwenye orodha ndefu ya wachezaji waliowahi kukumbwa na visanga vya imani za kishirikina baada ya Emanuel Adebayor ambaye hivi karibuni alimshutumu mama yake mzazi kwa kumroga.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook