Katika maisha kila mtu ana malengo na mipango yake, hata tukija katika ishu za kutafuta mchumba au kuoa kila mtu ana vigezo vyake, basi mimekutana na kigezo cha mmoja kati ya rapper wakali kutoka Nigeria ambaye jina lake la kuzaliwa ni Jude Abaga ila mtaani anafahamika kama Mr Incredible (MI).
MI Abaga ambaye ni CEO wa record label ya Chocolate City, ametaja moja kati ya kigezo chake atakachokitumia wakati atakaoamua kuoa mwanamke mweupe, nu kuomba picha yake ya utoto ili athibitishe kuwa mwanamke aliyeamua kuoa ana ngozi yake ya asili na vigezo kadhaa.
“Ukizungumzia sifa za mwanamke gani nataka, kwanza awe mrefu ili ata tukipata watoto wakitokea warefu sio mbaya kwa sababu mimi sio mrefu, kingine lazima niombe kuona picha yake ya utoto ili niangalie kuwa rangi ya mgozi yake ni ya asili au sio ya asili, maana wanawake wengi siku hizi hawana rangi ya ngozi zao za asili, baada ya hapo ndio tutaamua kuwa pamoja” >>> M.I
Mtu wangu kama utakuwa unakumbuka vizuri MI ndio jamaa ambaye record label yake inamsimamia Victoria Kimani wa Kenya, lakini pia staa huyo wa hit single za Crowd Mentality na Real Man alikuwa pamoja na mkali wa Bongo Fleva Diamond Platnumz katika Coke Studio Season One.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.