Kila mmoja ana ndoto ya baadae juu ya maisha sasa basi hapa ninayo stori ya msanii kutoka Weusi Nikki wa pili ambaye yeye ndoto yake ni kuhakikisha wasanii wenzake wanapata misingi sahihi ikiwemo mapato yanayotoka kwenye makampuni mbalimbali.
Msanii huyo aliizungumzia ndoto yake kwenye mdahalo wa vijana uliofanyika hivi karibu katika hoteli ya New Africa Dar es Salaam na kusema..’Ndoto ya msanii ni kwamba haujutii kuzaliwa na kipaji chako hapa Tanzania kama unakipaji kuwe na mazingira yote yanayo support kipaji chako kuwe na mafunzo kuwe na sera, kuwe na sheria, taasisi masoko hivyo vitu vyote vina support kipaji chako kutoka kwa kile kiwango mwenyezi Mungu alivyokujaalia kama si msanii una ndoto yako au mtu wa kawaida kuwe na mazingira ambayo yanaweza kukusaidia kwa viwango sawa upate maarifa ia uwe unashiriki kwenye uchumi pia una na nyezo za kushiriki kwenye uchumi
‘Ndoto yetu sisi wasanii kuhakikisha sekta ya muziki inakuwa namba moja katika upande wa uchumi tunataka miundombinu ya sanaa tunataka watunga sera kuanzia Serikali za mitaa level ya wilaya wakati wanatunga sera zao za kimaendeleo za kiuchumi waigize picha ya sanaa katika sera kwasababu miundombinu ya sanaa haipo’ – Nikki wa pili
Unaweza uka bonyeza play kumsikiliza Nikki wa pili akizungumzia ndoto yake kwa sanaa ya Tanzania.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos