Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya kazikubwa sana kuhakikisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) unaweza kulipa mafao stahiki na endelevu.
Akizungumzia juu ya Mfuko huu, Waziri Mkuu Mstaafu waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda baadaya kutembelea banda la WCF wakati wa Maonesho ya 46 yaKimataifa ya Viwanda na Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) amesema Serikali ya Awamu ya Nne ilianzisha Mfuko huu ilikutatua changamoto zilizokuwa zikiwakabili waajiri hususan waSekta Binafsi ambao walilazimika kupoteza muda mwingiwakati wafanyakazi wao walipopatwa madhila yaliyotokana nakazi.
Mhe. Pinda ametoa wito kwa waajiri wote nchini kuchangamkiafursa kwa kujiunga na kuwachangia wafanyakazi wao WCF ilikulinda biashara zao na wafanyakazi wao. Amesema, kuna kazikubwa ya kuelimisha waajiri na wafanyakazi nchini ili kufahamukwa ufasaha nini wanaweza kupata kutoka WCF.
Amepoungeza Mfuko huo kwa kuweka misingi imara namadhubuti iliyowezesha Shirika la Kazi Duniani ILO kuthibitisha uwezo wa Mfuko huu katika ulipaji wa fidia stahikikwa wanufaika wake kwa zaidi ya miaka 30 ijayo.
“Nimefurahishwa na tathmini ya ILO kuhusu uhai wa WCF naulipaji wa fidia ikiwemo malipo ya pensheni kwa wafanyakaziwaliopata ulemavu wa zaidi ya asilimia thelathini (30) na wenzawa wafanyakazi waliofariki kutokana na kazi. Hili ndio lengohaswa la kuanzishwa kwa Mfuko huu na Serikali inajivunia sanakuona matunda ya kuanzishwa kwake” alisisitiza, Mhe. Pinda.
Mhe. Pinda ameongeza kuwa malipo ya fidia kwa wafanyakaziyanaleta hamasa kwa waajiri wote nchini pamoja na wawekezajikwani kwa kufanya hivyo, Tanzania inakuwa kituo sahihi cha biashara na uwekezaji.
Naye Naibu Waziri Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb), amewahimiza waajiri wotenchini kuchangia WCF ili wafanyakazi wao wanufaike nahuduma zinazotolewa na Mfuko endapo wataumia, kuugua amakufariki kutokana na kazi.
“Jitahidini mjiunge na WCF na muione hii kama fursa kwenu nasio mzigo kwa sababu itawapunguzia malalamiko yasiyo yamsingi endapo wafanyakazi watapata ajali, ugonjwa au kifokutokana na kazi,” amesisitiza Mhe. Kikwete.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt. John Mduma amesemaWCF itaendelea kufidia wafanyakazi waliopata ulemavukutokana na kazi pamoja na wategemezi wa wafanyakaziwaliofariki kutokana na kazi.