Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amewashauri Watanzania kutorudi nyuma kwenye vita dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona na badala yake waendelee kuchukua tahadhari kama ambavyo Majeshi mbalimbali huwa yanajiandaa kukabiliana na maadui.
Chalamila ametoa kauli hiyo wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe cha kupokea na kujadili hoja zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambapo amesema viongozi wa Serikali ndio wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kwenye vita hiyo.
CORONA: MCHUNGAJI AWAVAA WASIOVAA MASK KANISANI “CORONA INAPIGA MWILI SIO ROHO MSINIANGALIE MIMI”