Kuna msemo usemao ‘Hujafa Hujaumbika’, Mishaly Sumary ni mwanamke wa Kitanzania aliyejawa na ndoto kubwa lakini ghafla alikuta zinakatika kutokana na kushambuliwa na watu Wasiojulikana waliomsababishia matatizo ya Kiafya yaliyomfanya maisha yake yawe na Kitandani huu ukiwa ni mwaka wa Nane (8).
Ayo Tv na Millardayo.com imefunga safari hadi Kibaha mkoani Pwani kwa ajili ya kuzungumza na Mishaly ambaye anahitaji msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo fedha kwa ajili ya kumsaidia arudi nchini India kwa mara ya pili kwa ajili ya matibabu.