Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imefungua zabuni kwa ajili ya kushindanisha kampuni tatu kubwa za Kimataifa ili kumpata mmoja atakayejenga mradi wa barabara ya mwendo wa haraka (Kibaha – Mlandizi – Chalinze – Morogoro Express Way) yenye urefu wa kilomita 205 kwa utaratibu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na binafsi (PPP), sehemu ya kwanza Kilomita 78.9 kutoka Kibaha – Mlandizi hadi Chalinze.
Katika Mahojiano na Ayo TV, Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) David Kafulila ameeleza mpango wa Serikali katika kufungua mlango ya uchumi kwa Jiji la Dar es salaam pamoja na Dodoma na kuwa litakwenda kuweka alama kubwa nchini.