Moja kati ya habari za soka zinazochukua headlines kwa sasa katika mitandao mbalimbali ni pamoja na hii ya Rais wa chama cha soka nchini Palestina, Jibril Rajoub kufungiwa miezi 12 kujihusisha na soka.
Jibril Rajoub amefungiwa na shirikisho la soka duniani FIFA kwa kosa la kushawishi watu wachome moto jezi za staa wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, kama sehemu ya kupinga kuchezwa kwa mchezo wa kirafiki kati ya Argentina dhidi ya Israel.
Rais huyo alikuwa anapinga mpango wa game ya Argentina na Israel kuhamishwa kutoka Haifa hadi Jerusalem, hivyo akawashawishi watu wachome jezi zenye jina la Messi kama staa huyo ataenda kucheza katika game hiyo.
Jibril Rajoub atatumikia adhabu hiyo pamoja na faini ya pound 15826 licha ya kuwa game ya Israel na Argentina iliahirishwa kutokana na Argentina kuhofia usalama wa wachezaji wao, Israel na Palestina wamekuwa hawako katika mahusiano mazuri kwa muda mrefu.
Samatta hataki utani safari ya Europa League, leo kapiga hat-trick