Baada ya uongozi wa klabu ya Simba kutangaza kumfukuza kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo muingereza Dylan Kerr na kocha wa makipa Iddi, January 18 makumu wa Rais wa klabu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu ametangaza ni kweli wapo katika mchakato wa kuongeza nguvu katika benchi la ufundi kwa kumuongeza kocha msaidizi wa Taifa Stars Hemed Morocco.
Kaburu amethibitisha kuwa Morocco atakuwepo kama kocha na mshauri wa timu ya Simba kwa kipindi hiki inachofundishwa na kocha mganda Jackson Mayanja, ila hawajaitangaza sana kwa sababu bado mambo hayajakaa vizuri na hawawezi kuweka mambo ambayo bado hayajakamilika.
“Jambo hilo ni kweli lakini bado hatujaliweka nje kwa maana ya kulijadili, kwani mambo bado, ni kweli tunamuhitaji Morocco ambaye pia ni muajiriwa wa TFF, ila wakati huu ambao tupo kwenye mchakato wa kutafuta kocha mkuu, tuliona kwamba kuna haja ya kuongeza nguvu katika benchi letu la ufundi” >>> Geofrey Nyange
Kwa upande wa Hemed Morocco amethibitisha kuwepo mpango huo, ambao kwa upande wake amesema kuwa mpango ulianzia Zanzibar lakini leo January 18 alikuwa asaini mkataba sema kipengele cha mshahara kilikuwa tofauti na walivyokubaliana awali hivyo anawapa muda wafikirie.
“Suala hilo ni kweli lakini naona kama bado hatujaafikiana, suala la upande wa maslahi kwani tulikuwa hatua za mwisho lakini suala la mshahara likabadilika dakika za mwisho, kitu ambacho tulikuwa tumekubaliana toka Zanzibar, Rais mwenyewe naona kama kabadilika flani hivi, mimi nilikuwa tayari kwenda kuifundisha Simba” >>> Morocco
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.