Mwimbaji mahiri wa Afrika Kusini Tyla atachuana tena uso kwa uso na wababe wa Afrobeats wa Nigeria katika Tuzo za Muziki za MTV za 2024 zinazotarajiwa kufanyika Septemba 11.
Mwimbaji huyo wa ‘Water’ ameteuliwa katika kitengo cha Best Afrobeats pamoja na nyota wa Nigeria Ayra Starr, Burna Boy, na Tems.
Nyota hao wa Kiafrika kwa pamoja lazima washinde ushindani mkali kutoka kwa watumbuizaji wa Marekani Chris Brown na Usher, ambao wote wameteuliwa katika kitengo cha Afrobeats.
Usher ameteuliwa kwa ushirikiano wake na mtayarishaji wa rekodi, mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Nigeria Pheelz katika wimbo mmoja wa “Ruin.”
Chris Brown kwa upande wake, ameteuliwa baada ya kushirikiana na watumbuizaji wa Nigeria Davido na Lojay katika wimbo wa “Sensational.”
Tyla ambaye ni mshindi wa Grammy pia yuko katika kinyang’anyiro cha tuzo katika vipengele vya Msanii Bora na Msanii Bora wa Rhythm & Blues, ambapo anashindana na waimbaji mashuhuri kama vile Alicia Keys na Usher.
Mwimbaji nyota wa kimataifa Taylor Swift anaongoza kundi hilo kwa kuteuliwa mara 10, zikiwemo Msanii Bora wa Mwaka, Wimbo Bora wa Mwaka na Video Bora ya Mwaka.
VMA za 2024 zitafanyika nchini Merika mnamo Septemba 11 kwenye Ukumbi wa USB huko New York.