Wawili hao walitoa taarifa yao kubwa kwenye ukurasa wa Instagram siku ya Jumapili, baada ya Megan kusambaza picha yake na kipa huyo wa Everton wakiwa wamesimama ufukweni huku akimpapasa mtoto wake.
Katika picha hiyo, Pickford mwenye umri wa miaka 29, mlinzi anaonekana akiwa amemkumbatia mrembo huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye alivalia vazi lililoonyesha wazi tumbo lake.
“”Adding one more for us to adore. We can’t wait for you baby.” alinukuu kwenye post hiyo.
Picha nyingine kwenye post hiyo inawaonyesha Jordan na Megan wakiwa wamesimama na mtoto wao Arlo, ambaye uso wake ulikuwa umefunikwa na emoji ya kopa ili kulinda faragha yake.
Wanandoa hao walioana mnamo 2020 walipokutana na kuanzisha mahusiano yao na kupata mtoto wakwanza