Game ya Azam Sports Federation Cup ya Yanga SC dhidi ya Iringa United uwanja wa Uhuru ilikuwa gumzo baada ya mchezo kulazimikakusimama kwa dakika kadhaa baada ya dakika ya 52 kutokea sintofahamu.
Wakati mchezo huo Yanga walioshinda 4-0 na kuitoa Iringa ukiendelea, kulizuka taharuki uwanjani hapo na wachezaji kulazimika kulala chini kufuatia kuzuka kwa nyuki na kusababisha mchezo kusimama huku wachezaji na waamuzi wakilala chini.
Hakuna madhara makubwa zaidi yaliyojitokeza hadi sasa yaliyoripotiwa na mchezo huo uliendelea na Yanga kumaliza kwa ushindi mnono wa 4-0 zikifungwa na Papy Tshishimbi dakika ya 8, Patrick Sibomana dakika ya 10, Lamine Moro dakika ya 39 na David Molinga dakika ya 70.