Kupitia kwenye ukurusa wa Instagram wa Jacqueline Mengi, amepost video ambayo inaonyesha namna ambavyo sehemu ya nyumba yake ilivyopata majanga ya kuingiliwa na maji kufuatia Mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam.
Katika maneno ambayo ameyaambatanisha katika video hiyo ameonyesha hisia zake za kupoteza vitu vyenye kumbukumbu nyingi kwenye maisha yake.