Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), limeonya kuwa nzige walio Kusini mwa Ethiopia wanaanza kusambaa kuelekea katika mataifa ya Afrika Mashariki.
FAO katika ripoti yake iliyotolewa leo, inasema nzige hao wameanza kuonekana Mashariki mwa Ethiopia na baadhi ya maeneo ya Somalia, kuelekea Kaskazini Mashariki mwa Kenya.
Tayari nzige hao wapo katika kaunti za Kenya za Wajir, Garisa na Marsabit lakini wenine wameonakana katika kaunti ya Taita Taveta, karibu na Tanzania.
Shirika hilo linaonya kuwa, kuendelea kuwepo kwa nzige hao kunatishia usalama wa chakula katika eneo la Afrika Mashariki, baada ya mwaka jana nchi za Afrika Mashariki kuharibu mabilioni ya wadudu hao.