Rais Obama amekosoa baadhi ya sheria zilizowekwa na majimbo na nchi mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.
Obama amekosoa kuhusiana na sheria ya kuweka karantini siku 21 manesi na madaktari waliotoka nchi za Afrika Magharibi kuhudumia wagonjwa wa Ebola kwa kusema kuwa sheria hiyo inawavunja moyo watu hao walioamua kujitolea maisha yao kwa kuwasaidia waathirika wa ugonjwa huo.
Rais huyo hakutaja majina ya majimbo wala nchi ambazo anazikosoa kwa sheria hizo kandamizi, lakini New York na New Jersey zilitangaza utaratibu huo ambao ulianza kutekelezwa mwanzo wa wiki hii hivyo inaonekana ujumbe wa Obama umelenga magavana wa majimbo hayo.
Kauli ya Obama huenda ikawa na tafsiri inayokosoa vilevile uamuzi uliofanywa na serikali ya Australia wa kuzuia kuingia nchini humo mtu yoyote anayetokea ukanda wa nchi za Afrika Magharibi ambazo zimeathiriwa zaidi na janga la ugonjwa huo.