Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imemsimamisha Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia na Sekretarieti yake yote kutojihusisha na siasa ndani ya Chama hicho hadi uamuzi huo utakapoamuliwa vinginevyo.
Uamuzi huo unakuja siku chache baada ya Halmashauri Kuu ya Chama hicho kumsimamisha Mbatia na Makamu Mwenyekiti Bara Angelina Mtaigwa kujihusisha na shughuli zozote za Chama hicho mpaka watakapoitwa kujieleza katika mkutano Mkuu wa Wanachama wa Chama hicho, uamuzi ambao hata hivyo Mbatia na wenzake waliupinga.
MANARA AWEKA WAZI KUHUSU MORRISON KUTUA YANGA ‘WAO WANAHISI TUNAMSAJILI, HATUNA MIPANGO HIYO’