Leo Febrary 12, 2019 nakusogezea mambo sita ya kuzingatia kwako wewe mtumiaji wa simu hasa huduma za kifedha, mtumiaji wa huduma za kifedha mtandaoni unashauriwa kuzingatia yafuatayo:
1. Usiweke kiwango kikubwa cha pesa kwenye akaunti ya fedha kwa mtandao kwa muda mrefu. Tumia huduma za Benki kutunza kiasi kikubwa cha fedha, na unapozihitaji kwa kufanya miamala, basi unaweza kuzitoa huko na kuziingiza kwenye simu kwa ajili ya matumizi yako mtandaoni.
2. Tumia namba ya siri ambayo sio rahisi mtu mwingine kukisia. Usitumie mwaka wako wa kuzaliwa au wa mtu wa karibu kama mwenza au watoto. Ni vyema kuibadili namba hiyo mara
kwa mara.
3. Thibitisha na hakiki namba ya mtu unayemtumia pesa au salio kabla ya kutuma. Hapa tunasisitiza, hakikisha, hakikisha na hakikisha tena kabla ya kukamilisha muamala.
4. Usimpe mtu yeyote usiyemfahamu vizuri simu yako au kadi yako ya simu ili atumie.
5. Usitoe namba zako za siri au taarifa zako binafsi unazotumia kwa huduma za kimtandao kwa mtu yeyote, (hapa tunasisitiza usitoe kwa mtu yeyote) kwani anaweza kutozitunza vyema au yeye mwenyewe akazitumia kwa utaratibu ambao hujauridhia.
6. Ukipigiwa simu au kutumiwa ujumbe mfupi unaokuelekeza kutuma fedha, hata kama mtu
anayekuagiza unamfahamu hakikisha kuwa ndiye kabla ya kutekeleza maagizo hayo. Usishinikizwe
na maelekezo ya ujumbe mfupi (sms), kwa kuwa wahalifu wana njia nyingi za kulaghai. Ukiwa
hujajiridhisha, mpigie simu aliyekutumia ujumbe
RAHA KIBANDA UMIZA: TAZAMA SHANGWE ZA GOLI LA KAGERE DHIDI AL AHLY