Wiki iliyopita Tume ya Vyombo vya Habari Rwanda (RMC) ilisema wiki hii itafanyia kazi madai kuhusu maoni yaliyotolewa dhidi ya wanawake na Mhubiri kwenye kituo kimoja cha redio nchini humo.
Malalamiko hayo yalitolewa na kikundi cha wanawake wanaharakati wa masuala ya wanawake waitwao Pro – Femmes Twese Hamwe. Wanawake hao wamemshtaki Mhubiri huyo kwa kusema ‘wanawake ni chanzo cha maovu’.
Leo ikiwa ni Siku ya Redio Duniani, mamlaka hiyo imeamuru kufungwa kwa kituo hicho cha radio kwa kipindi cha miezi mitatu kama adhabu ya kile kilichotokea.
Ilivyokuwa katika kesi ya mauaji ya Mwanaharakati wa Tembo
“Nawatakia kazi njema, kafanyeni kazi” -Rais Magufuli