Okwi ni Miongoni mwa wachezaji walionekana kuzongwa na maelezo mengi ikiwa ni pamoja na kusimamishiwa uhamisho wake mara baada ya kujiunga na club ya Yanga sasa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa taarifa rasmi.
Taarifa kutoka TFF imewalalamikia wana familia watano wa shirikisho hilo la mpira wa miguu kwa Kamati ya Maadili kuhusiana na udanganyifu katika mtihani wa utimamu wa mwili wa waamuzi na usajili wa mchezaji Emmanuel Okwi.
Wanafamilia wa Tff wanaotuhumiwa ni pamoja na Riziki Majala na Army Sentimea ambao ni wakufunzi wa waamuzi,Oden Mbaga na Samwel Mpenzu ambao ni waamuzi wanadaiwa kughushi nyaraka kuhalalisha mtihani huo kinyume cha taratibu.
Mtu mwingine anaetuhumiwa juu ya sakata hili ni Sabri Mtulla ambaye analalamikiwa na TFF kwa madai ya kuidanganya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuwa hakukuwa na pingamizi lolote juu ya usajili wa mchezaji Emmanuel Okwi huku akijua wazi kuwa jambo hilo si kweli.
Kwa mujibu wa kanuni malalamiko hayo yamefikishwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo itachunguza ili kujiridhisha kama yana msingi au la,ikibaini kuna kesi ndipo walalamikiwa watafika mbele ya kamati hiyo.