Aliwahi kusikika staa wa Bongofleva kitambo ambaye kaamua kurudi tena kwenye game, Q Chief akiongelea kutofautiana na Management yake ya muziki inayoongozwa na Q S Mhonda.
Leo unasikika upande wa pili, Manager mwenyewe Mhonda amesema Q Chief alimtafuta, wakakaa wakaongea na kila kitu kikawa sawa kwa hiyo ile ishu ya tofauti zao haipo tena.
Kuna watu wanaweka nguvu nyingi sana kuwa mastaa, lakini kuna mastaa wako kwenye kona wasiyoipenda kutokana na ustaa… mmoja wao ni Jux, jamaa anasema kuna wakati anauchukia ustaa, mfano wakati wa kesi ya mpenzi wake Jackline kukamatwa China, watu walimnyooshea kidole kwa sababu ya ustaa wake.
Jux anasema kuna wakati mwingine hawezi kuwa huru kwenye maisha yake kwa sababu tu ni staa wa muziki.
Joh Makini amesema toka anaanza game yake ya hiphop alihitaji kuwa kwenye level yake palepale, haoni kama kuna umuhimu wa kushindanishwa na rappers wengine ndio maana hakuwahi kumzungumzia msanii yoyote vibaya.
255 hii hapa kwenye audio na stori zote niliyorekodi kwenye XXL ya leo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.