Shirikisho la soka Duniani (FIFA), limetoa orodha ya wanasoka 11 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Dunia 2020, tuzo hiyo itatolewa Disemba 17, 2020, sambamba na tuzo ya kocha bora, wa kike na wakiume, golikipa bora na goli bora la mwaka.
Katika orodha hiyo mabingwa wa England klabu ya Liverpool ndio imeongoza kwa kutoa wachezaji wengi kwenye orodha hiyo, imetoa wachezaji 4 ambao ni Thiago Alcântara, Sadio Mané, Mohamed Salah, na Virgil van Dijk.
Wachezaji wengine wanaowania tuzo hiyo ni Cristiano Ronaldo, Kevin De Bruyne, Robert Lewandowski, Kylian Mbappé, Lionel Messi, Neymar, na Sergio Ramos . Mwaka jana 2019 tuzo hii alishinda mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi.
Makocha wanaowania tuzo ya kocha bora ni Marcelo Bielsa wa Leeds United FC, Hans- Flick wa FC Bayern München, Jürgen Klopp Liverpool FC, Julen Lopetegui wa Sevilla FC na Zinedine Zidane waReal Madrid CF.
Wanao wania tuzo ya Golikipa bora ni
Alisson Becker wa Liverpool FC
Thibaut Courtois wa Real Madrid CF
Keylor Navas wa Paris Saint-Germain
Manuel Neuer wa FC Bayern München
Jan Oblak wa Atlético de Madrid)
Marc-André ter Stegen wa FC Barcelona
Tuzo ya mchezaji bora wa kike inawaniwa na.
Lucy Bronze ( Olympique Lyonnais / Manchester City WFC)
Delphine Cascarino (France / Olympique Lyonnais)
Caroline Graham Hansen ( FC Barcelona)
Pernille Harder ( Chelsea FC Women)
Jennifer Hermoso ( FC Barcelona)
Ji So-yun ( Chelsea FC Women)
Sam Kerr ( Chelsea FC Women)
Saki Kumagai ( Olympique Lyonnais)
Dzsenifer Marozsán ( Olympique Lyonnais)
Vivianne Miedema ( Arsenal WFC)
Wendie Renard ( Olympique Lyonnais)
Tuzo ya kocha bora wa timu za wanawake
Lluís Cortés wa FC Barcelona
Rita Guarino wa Juventus Women
Emma Hayes wa Chelsea FC Women
Stephan Lerch wa VfL Wolfsburg
Hege Riise wa LSK Kvinner
Jean-Luc Vasseur wa Olympique Lyonnais
Sarina Wiegman wa timu ya taigfa ya Uholanzi