Staa wa ngumi duniani raia wa Ufilipino Manny Pacquiao amesema anatarajia kustaafu mchezo huo April 2016 baada ya kumaliza pambano lake na bondia Timothy Bradley.
Bondia huyo ambaye tayari ameshinda mataji nane ya ubingwa wa dunia kwa sasa ana ndoto za kuwania nafasi za juu za uongozi katika nchi yake ya Ufilipino pia anaamini ana nafasi kubwa ya kuiongoza nchi hiyo.
Pacquiao atapambana na bondia huyo kutoka America kwa mara ya tatu April 9, 2016 ikiwa ni baada ya kushindwa kumudu kumpiga mpinzani wake mkubwa Floyd Mayweather katika pambano lililofanyika Las Vegas hivi karibuni.
“Natarajia kustaafu ngumi na kujikita zaidi kwenye mambo ya siasa, pambano langu la mwisho litakuwa dhidi ya Timothy” alisema jana katika mahojiano.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.