Michezo

Pamoja na kupoteza Samatta ana wastani mzuri wa magoli Champions League

on

Mtanzania Mbwana Samatta licha ya timu yake ya KRC Genk kupoteza kwa kufungwa magoli 4-1 dhidi ya RB Salzburg katika mchezo wao wa tano wa UEFA Champions League, Samatta anaendelea kujiweka sokoni kutokana na kuendelea kufunga.

Katika mchezo wao wa tano akicheza na KRC Genk Champions League ambapo tayari wameshaondolewa, Samatta alifunga goli la kufutia machozi dakika ya 85 na hilo kuwa goli lake la tatu Champions League akicheza jumla ya michezo mitano, kitu ambacho kitamuweka pazuri katika dirisha la usajili la mwezi January kiasi cha kuweza kuonekana na timu mbalimbali.

Matokeo mengine ya November 27 2019.

VIDEO: Samatta baada ya kupokea comments zinazodai hachezi vizuri Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments