Magazeti

Stori kubwa kwenye uchambuzi wa Magazeti April 21 2016…#PowerBreakfast (+Audio)

on

April 21 2016 millardayo.com imekurekodia uchambuzi wa magazeti kutoka Power Breakfast ya Clouds FM, ni uchambuzi wa Habari zote kubwa kupitia magazeti yaliyoandikwa leo Tanzania, Hizi ni baadhi ya Habari kubwa zilizoandikwa leo.

Uamuzi wa JPM kwa Kabwe wakosolewa, Rais John Magufuli anaendelea kujipatia umaarufu kutokana na vitendo vyake vya kusimamisha kazi na kutimua watumishi wa umma, lakini uamuzi wake wa ‘kumtumbua’ Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam , Wilson Kabwe haujapokelewa vizuri na wadau ambao baadhi wameonya kuwa ni hatari nchi kuendeshwa kishabiki.

Serikali yashtuka mizigo kupungua bandarini, Hatua ya wasafirishaji wa nchi jirani wanaotumia bandari ya Dar es salaam kuisusa bandari hiyo imeishtua Serikali, ambayo imeamua kuunda kikosi kazi maalumu kwa ajili kutafuta namna ya kunusuru hali hiyo.

Gari latumbukia baharini laua, Watu wawili wamepoteza maisha, baada ya gari walilokuwa wakitumia kudondoka kwenye kivuko cha MV Kigamboni kilichokuwa kikitoka Feri kuelekea Kigamboni na kutumbukia baharini

Unaweza ukasikiliza sauti hapa chini…

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

JINSI ALIVYOAGWA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA UTUMISHI BOT APRIL 20 2016 NA WATU WALIOPEWA RUHUSA…

Soma na hizi

Tupia Comments