November 6 2015 tayari ninazo zote nilizozinasa kwenye Uchambuzi wa Magazeti Redioni, hizi hapa kwenye nukuu yake pamoja na audio niliyorekodi.
Rais Dk. Magufuli amesema yeye ndiye Rais, akiri uchaguzi ulikuwa mgumu na amejifunza mengi… Changamoto za uongozi wa Dk. Magufuli zatajwa.
Rais JPM ameanza kazi kwa kumteua George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu Tanzania, Mawaziri Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye hawakuhudhuria sherehe za kuapishwa Dk. Magufuli, wapingana na matokeo ya Urais.
Mawaziri na Manaibu waliomaliza muda wao warudisha ‘MASHANGINGI’ Ikulu ili yatolewe namba na kufanyiwa matumizi mengine… Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad bado hajarudisha magari ya Serikali japo alisema hadi Novemba 2 2015 Z’bar itakuwa haina Serikali.
JK atoa msamaha kwa wafungwa 4,100 muda mfupi kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais JPM… Majambazi yateka magari Tabora na kupora watu huku wakiimba ‘hapa kazi tu’!!
Aliyekuwa Askari Polisi Oysterbay amehukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha…
Stori zote ziko kwenye audio niliyorekodi pia mtu wangu.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.