Mchungaji Mmarekani ambaye anaishi nchini Uturuki anashtakiwa kwa tuhuma za kusaidia kikundi cha ugaidi kufanya matukio ya kigaidi nchini humo.
Mchungaji huyo anayejulikana kwa jina la Andrew Brunson anadaiwa kusaidia kikundi hicho ambacho kinaongozwa na Fethullah Gulen ambaye ni kiongozi wa Kiislamu aliyepelekwa uhamishoni na mamlaka za Uturuki.
Kikundi hicho cha ugaidi kinasemekana kupanga mbinu za kuipindua serikali ya Uturuki mwaka 2016 lakini hata hivyo ilishindikana.
Mchungaji huyo Brunson ambaye ana umri wa miaka 50, akikutwa na hatia ya kosa hilo, inaelezwa kuwa atahukumiwa kifungo cha hadi miaka 35.
Mbowe, Viongozi 8 wa CHADEMA walivyofika Mahakamani kisutu leo