Baada ya klabu ya Manchester City kumsajili Raheem Sterling kwa ada ya uhamisho wa pound million 49 kutokea klabu ya Liverpool, kumekuwa na maoni mbalimbali kuhusiana na kiwango hicho cha fedha kuwa ni kikubwa na bado mchezaji huyo hajafikia thamani hiyo.
Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrin amejibu hivi>>>>> “Bei sio kitu muhimu sana, kitu muhimu ni kuchagua aina ya mchezaji unayemuhitaja… siku zote unapohitaji mchezaji bei huwa ipo juu hii sio kwa Man City pekee hata timu zingine”>>>>Pellegrin
“Nafikiri Raheem anaweza kucheza nafasi tofauti tofauti, anaweza kucheza kama mshambuliaji sababu ana kasi sana au anaweza kucheza kama winga”>>>Pellegrin
“Ni bado mchezaji mdogo hivyo ana vitu vingi vya kujifunza, nafikiri ni wakati sahihi wa yeye kupata changamoto mpya katika timu yetu ambayo atacheza na wachezaji wakubwa na kuimarisha kiwango chake”>>>>Pellegrin
Sterling ameingia katika rekodi ya kuwa mchezaji mdogo mwenye thamani zaidi Uingereza baada ya kuhamia Man City akitokea Liverpool kwa ada ya uhamisho wa pound million 49.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.