Kocha wa klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani Pep Guardiola ambaye pia anahusishwa kutaka kujiunga na vilabu vya Man United, Chelsea na kwa kiasi kikubwa Man City, December 28 aliwasili uwanja wa ndege wa Kenya JKIA kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu ya mwaka mpya.
Uwepo wa Guardiola Kenya ambapo amepokelewa na Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho, unatafsirika kama kwenda kupumzika na kutafakari ofa za vilabu vya Ulaya vinavyomuhitaji. Guardiola tayari amethibitisha kuwa hatoendelea kuifundisha FC Bayern Munich na anatajwa kusaini mkataba wa awali.
“Kiukweli anafuraha kuwa Kenya na familia yake, Pep anasema atakuwa Kenya hadi mwaka mpya lakini anahitaji kuishi maisha ya kawaida tu na kujipumzisha na familia yake” >>>Ali Hassan Joho
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.