Serikali ya Marekani imeeleza kuwa itaanza kukusanya taarifa za mitandao ya kijamii ya watu wote watakaokuwa wanataka kuomba visa ya kuingia nchini humo.
Inaelezwa kuwa watu wote watakaokuwa wanaomba visa ya kuingia nchini Marekani itawabidi kutoa taarifa zao za mitandao ya Facebook pamoja na Twitter.
Utaratibu huu mpya utawalazimu kutoa majina yao ya akaunti zao za mitandao hiyo ambazo wamezitumia kwa miaka mitano kabla ya kuomba visa hiyo.
Suala hili linaelezwa kuwaathiri watu takriban milioni 14.7.
Rungwe amempata Binti yake alietekwa ameeleza alichoulizwa na Watekaji